26 August 2011

Matokeo mitihani ya walimu yatangazwa

Na Edmund Mihale

BARAZA la Mitihani nchini limetangaza matokeo ya walimu katika madaraja mbalimbali nchi katika mtihani uliofanyika Mei mwaka huu.Akitangaza matokeo hayo jana
Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Dkt. Joyce L. Ndalichako alisema kuwa umauzi wa kutangaza matokeo hayo ulifikiwa katika kikao chake cha 84 kilichofanyika Agosti 22 mwaka huu.

Kikao hicho kimeridhia kutangaza matokeo ya Mtihani wa Ualimu Daraja la A ngazi ya cheti(GATCE) Mtihani wa Ualimu Daraja la A – Kozi Maalumu (GATSCCE) Mtihani wa Stashahada ya Ualimu Sekondari (DSEE) na Mtihani wa Stashahada ya Ualimu Ufundi (DTE), alisema Dkt. Ndalichako.

Alisema kuwa katika mitihani hiyo watahiniwa waliosajiliwa kufanya mtihani wa Ualimu Daraja A ni 10,887.  Wasichana walikuwa ni 5,621 sawa na asilimia 51.63 na wavulana ni 5,266 sawa na asilimia 48.37 ya watahiniwa wote waliosajiliwa.

Alisema kuwa kati ya watahiniwa waliosajiliwa, watahiniwa 10,852 walifanya mtihani, wakiwemo wasichana 5,604 (99.70%) na wavulana 5,248 (99.66%). Watahiniwa 35  (0.32%)  hawakufanya mtihani, kati yao wasichana ni 17 (0.30%) na wavulana ni 18 (0.34%).
   
Alisema kuwa watahiniwa waliosajiliwa kufanya mtihani wa Daraja la A -Kozi Maalumu ni 265. Wasichana walikuwa ni 152  sawa na asilimia 57.36  na wavulana ni 113 sawa na asilimia 42.64 ya watahiniwa wote waliosajiliwa.

"Kati ya watahiniwa waliosajiliwa, watahiniwa 263 walifanya mtihani, wakiwemo  wasichana  151 (99.34%) na wavulana 112 (99.12%). Watahiniwa wawili (2) sawa na asilmia 0.75  (msichana mmoja  na mvulana mmoja) hawakufanya mtihani aliasema Dkt Ndalichako.   

Alisema kuwa watahiniwa waliosajiliwa kufanya mtihani wa Stashahada ya Ualimu Sekondari ni 7,239. Wasichana walikuwa 2,593 sawa na asilimia 35.82  na wavulana ni 4,646 sawa na asilimia 64.18  ya watahiniwa wote waliosajiliwa.

"Kati ya watahiniwa waliosajiliwa, watahiniwa 7,211 walifanya mtihani ambapo watahiniwa 2,580 (99.50%) ni wasichana na wavulana 4,631 (99.68%). Watahiniwa 28 (0.39%)  hawakufanya mtihani wakiwemo wasichana 13 (0.50%) na wavulana 15 (0.32%)" alisema Dkt. Ndalichako.

Alisema watahiniwa waliosajiliwa kufanya mtihani wa Cheti cha Ualimu  Ufundi ni 34  wakiwemo  wasichana  wanne (4)  na wavulana 30. Kati ya watahiniwa waliosajiliwa, watahiniwa 33  walifanya mtihani ambapo wasichana ni wanne (4)  na wavulana ni 29.

Alisema katika matihani huo watahiniwa ambao hawajalipa ada ya baraza limesitisha kutoa matokeo ya watahiniwa 27 wasiolipa ada amboa ni sita katika ngazi ya GATCE na 21 DSEE

Alisema kuwa matokeo ya watahiniwa hao yatatolewa mara baada ya kulipa ada na faini wanayodaiwa.  Iwapo malipo hayo hayatafanyika katika muda wa miaka miwili (2) tangu tarehe ya kutangazwa kwa matokeo, matokeo yao yote ya mtihani yatafutwa  kwa mujibu wa kifungu 52 (b) cha Kanuni za Mitihani.

Alisema kuwa baraza hilo  limesitisha kutoa matokeo ya Mtihani ya watahiniwa saba  ambao sifa zao  za usajili zilikuwa na utata.  DSEE watahiniwa  wanne  na GATSCCE  watatu.




11 comments:

  1. MATOKEO YA MITIHANI KWA STASHAHADA NI MATUSI KWA WAKUFUNZI WANAFUNDISHA STASHAHADA NA GRADE "A" JE HAKUNA MWANAFUNZI WA STASHAHADA ANAWEZA KUPATA "DISTINCTION" MBONA NI WACHACHE SANA WAMEPATA"CREDIT" NA KADHALIKA GRADE"A" DISTINCTION SIFURI IWAPO NECTA HAITATOA SABABU ZA KISAYANSI KUHUSU MATOKEO HAYO SASA TUTATUHUMU WASAHIHISHAJI HAWAKO MAKINI SI AJABU HAWATUMII "MARKING SCHEME" BARAZA LITAKOSA SIFA

    ReplyDelete
    Replies
    1. Unae tukana kwamba walimu hawafundishi elewa kwamba vijana hamtaki kushauliwa na mnapoandika majibu mnafikiri mnamkomoa mwalimu kumbe munajiharibia maisha yenu wenyewe. Jichunguze kabla hujatoa lawama kwa mtu yeyote.

      Delete
    2. Tusipende kulaumu pasipo kufanya uchunguzi yakinifu,m/kiti wa CWT Gratian aliwahi kutoa ushauri kwa serikali kutowachagua wanafunzi wenye ufaulu duni kujiunga na vyuo hasa vyuo vya ualimu kwa ngazi zote.kama mwalimu mwanafunzi{student teacher]anafeli/ana supplimentary je,watoto atakaowafundisha watapata alama gani kama sio Div 0?

      Delete
  2. KUNA HAJA YA KUSUTA UTARATIBU WA USAHIHISHAJI IKIZINGATIWA WATAHINIWA WENGI HAWAGHARAMII MITIHANI YAO KUSAHIHISHWA UPYA KUTOKANA NA NECTA KUWEKA GHARAMA KUBWA ILI KUWATISHIA WASI"APEAL" MBONA WAISLAM WALIZOMEA NECTA WAKASAHIHISHA MTIHANI WA KIISLAM UPYA WASAHIHISHAJI WOTE NA UTARATIBU UTAZAMWE UPYA NECTA IJIKOSOE

    ReplyDelete
  3. HIVI SERIKALI INA MIKAKATI IPI MADHUBUTI KATIKA KUPANUA NA KUONGEZA IDADI YA WANAFUNZI WANAODAHILIWA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA UFUNDI? KUNA HAJA SASA YA NCHI KUONA UMUHIMU WA KUWA NA WATAALAMU WENGI WA KUTOSHA ILI KUENDANA NA MABADILIKO YA DUNIA YA SASA. MAANA KWA HALI KAMA HII YA WAHITIMU 33 HAIKIDHI AMA KUTOSHELEZA MAHITAJI YA UBORESHAJI WA ELIMU UKILINGANISHA NA IDADI YA WATANZANIA SASA.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kama vijana wenyewe wengi wanapenda kucheza disco watapendaje masomo yaufundi? Vyuo vya ufindi vipo walengwa waliopo hawafai hata kidogo wote ni wale ndugu zao wamewalazimisha kujiunga kwa lazima au akikataa anambiwa akatafute mzazi wake.

      Delete
  4. kwakweli ni majanga tena kwani kuna wanafunzi wamepata supp ikla GPA ni kubwa na wapo waliofaulu lakini GPA ni ndogo.je kuna uhalisia gani wa academic hapa?

    ReplyDelete
  5. Sifa walizoendea chuo = Matokeo yaliyotangazwa

    ReplyDelete
  6. NADHANI WALIMU WAMEAMUA,MAANA SERIKALI HAIJALI SECTA YA ELIMU KABISA, IWAPO JITIHADA ZA MAKUSUDI HAZITACHUKULIWA JANGA HILI LITAENDELEA KUATHIRI TAIFA KWA UJUMLA,NA NDO MSIBA NA SEKTA YA ELIMU TANZANIA WANAIZIKA BILA KUJIJUA.

    ReplyDelete
  7. IFIKIE WAKATI KILA MTU AJALI ULIO WAJIBU WAKE.HAKUNA MAENDELEO KIELIMU KAMA WAALIMU HAWATAJALIWA KIMASLAHI,VIONGOZI KUKUBALI USHAURI TOKA KWA WADAU WA ELIMU,WANAFUNXI KUKUBALI UDHAIFU NA KUKUBALI MAELEKEZO YA WAALIMU,NA KILA MTU KUMUELEKEA MUNGU MAANA ELIMU YATOKA KWA MUNGU MAANA MAANDIKO HUSEMA MSHIKENI SAANA HUYO ELIMU WALA USIMUACHE AENDE ZAKE NAAM MKAMATENI MAANA NDIO UZIMA WAKO.NI LAZIMA MAONI NA MAONYO VITOLEWE ILA KWA UPENDO SI KWA JAZIBA

    ReplyDelete
  8. NAOMBA PIA SWALA LA ELIMU KWA WATOTO WA WALEMAVU NA WALEMAVU WENYEWE IINULIWE MAANA KATI YA HAO WALIOFELI IDADI KUBWA NI YA WATOTO WA WALALA HOI WASIO NA HILI WALA LILE NATOA WITO TUSAIDIANE KUAIDIA KUNDI HILI.

    ReplyDelete