20 September 2012

CHADEMA sasa yamlima barua Rais Kikwete *Inamtaka awatimue kazi Nchimbi, IGP, Chagonji *Wamo RPC Moro, Iringa, pia yashauri iundwe tume *Akikaidi kushinikizwa kwa maandamano ya amani


Na Reuben Kagaruki

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimemwandikia barua, Rais Jakaya Kikwete, kikimtaka achukue hatua, kwa mujibu wa mamlaka yake kuchunguza mauaji yenye sura ya kisiasa yanayotokea nchini,


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na kusainiwa na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi, Bw.John Mnyika, barua ya chama hicho ya  Septemba 10, mwaka huu, iliandikwa na Mwenyekiti wa Taifa, Bw. Freeman Mbowe.

Barua hiyo inamtaka Rais Kikwete, achukue hatua ya kuwafukuza kazi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Emmanuel Nchimbi na Mkuu wa Jeshi la Polisi,IGP Said Mwema.

Wengine ni Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Polisi, Bw. Paul Chagonja, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Bw. Faustine Shigolile Kamanda wa Mkoa wa Iringa, Bw. Michael Kamuhanda, kwa kutowajibika kutokana na mauaji yaliyotokea katika mikoa yao.

Mbali ya kumtaka awawajibishe viongozi hao, pia CHADEMA, kimetaka Rais aunde tume ya Kijaji au Kimahakama ya uchunguzi
wa vifo vilivyotokea katika mikusanyiko, mikutano, maandamano au mazingira ya kisiasa yaliyohusisha CHADEMA.

Alitaja vifo hivyo kuwa ni vile vilivyotokea Arusha
Januari 5,mwaka jana, Igunga, Novemba, mwaka huo huo, Arumeru Mashariki vilivyotokea Aprili, mwaka huu.

Vingine ni vilevilivyotokea Iramba, Julai 14,  Morogoro Agosti 27 na Iringa Septemba 2, mwaka huu.

"Wakati tukisubiria hatua za Rais pamoja na majibu ya barua hiyo, CHADEMA kinawaagiza viongozi na wanachama wake kutokutoa ushirikiano kwa kamati iliyoundwa na Dkt. Nchimbi pamoja na timu zilizoundwa na Jeshi la Polisi kuchunguza mauaji yaliyofanywa na askari katika mikoa ya Iringa na Morogoro," alisema.

"Ili kupata ukweli wa sababu za vifo hivyo, mauaji yote haya hayajafanyiwa uchunguzi wowote wa Kimahakama au Kijaji kwa mujibu wa Sheria za nchi yetu, kinyume na ahadi ya Waziri Mkuu Bungeni wakati akihitimisha hoja yake katika Bunge la Bajeti la mwaka 2011/2012," alisema Bw. Mbowe.

Alisema  Kamati Kuu ya CHADEMA ilifanya hivi karibuni ilijadili hali ya siasa nchini kufuatia mfululizo wa mauaji yanayofanywa na Jeshi la Polisi na mipango ya baadhi ya viongozi wa Serikali ya kudhibiti vuguvugu la mabadiliko (M4C) kwa mbinu haramu.

Kamati kuu ilizingatia masuala mbalimbali na kupitisha maazimio nane na kuamua kumuandikia barua Rais kwa lengo la kumtaka achukue hatua za utekelezaji kwa mujibu wa mamlaka yake na kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

"Iwapo Serikali haitazingatia, CHADEMA kitawaongoza wananchi kwa njia za kidemokrasia ikiwemo maandamano ya amani kushinikiza hatua za haraka kuchukuliwa kwa maslahi ya taifa," alisema.

Bw.Katika majadiliano ya kina kabla ya kufikia maazimio na maamuzi hayo, Kamati Kuu ilizingatia kuwa hali ya siasa nchini ni tete, Serikali inayoongozwa na CCM imeshindwa kusimamia vizuri rasilimali za nchi ikiwemo kudhibiti mfumuko na ongezeko la bei.

4 comments:

  1. ni mtamo mzuri kwa masrai ya wananchi wa tanzania.
    ila najiuliza kila kukicha kwa nn mauji yote yaliyo tokea yahusu au yagusa chama kimoja?
    mimi naona chadema kwa siasa za chuki hazi tufai tena wasipo acha tuwa ogope maana hakuna sababu ya kufa eti kwa ajili ya mtu awe kiongozi tena ni bahati nasibu kufanya anayo ahidi.
    ni mtamo wangu

    ReplyDelete
  2. mimi nauliza.
    kwa nn michango ya hii vyama vyetu isitumike kwa ajili kutatua matatizo badala ya mikutano ya matusi na isiyo na mambo ya muhimu kwa taifa.
    hivi tujalibu kuangalia kama ingetumika kujenga miradi midogomidomo katika majimbo ya wambuni wa vyao hivyo.
    hizo ndo siasa za vitendo na sio kuongea tu na kuondoka wakati ya maisha ya watanzania inabaki balebale kila kukicha.
    mm naona uongozi usiwe kama majaribu bali uwe ni kufanya kazi tu.
    hivy kuna kila sababu ya wanasiasa hasa wapinzani wabadilike kwa kutekeleza baadhi ya miradi midogo kwa fedha za ruzuku, miradi na mapato ya misaada ya wafadhili wao wa chama kuliko kusubili mpaka wapewe dola huu ni unafiki mkubwa hakika hatuta endelea kamwe hata waje viongozi toka upinzani.
    tuyafanyie kazi kwani naamin ni msingi wa taifa letu kwa pamoja tuna weza.

    ReplyDelete
  3. Safi sana mheshimiwa MBOWE kwa barua yako ya kuwataka viongozi waliohusika wawajibishwe!. Mtazamo wangu ningefurahi sana km ningesikia viongozi wote wa CHADEMA walioratibu mikutano na maandamano yaliyosababisha vifo hivyo wangeanza wenyewe kuwajibika kwa kushindwa kuwatuliza wafuasi wao hasa pale wanapotakiwa kutii sheria bila shuruti ndipo meshimiwa Rais awawajibishe hao mliowataja. Mkifanya hivyo tutawaamini kuwa mmezamilia kuleta mageuzi ya kweli.Vinginevyo jiandaeni kudaiwa ndamu za watu zinazomwagika sasa kutokana na hamasa zenu wakati ninyi na familia zenu mnarudi nyuma kuangalia kitakachowapata ili mpate la kuongea

    ReplyDelete