28 December 2012

Mgonjwa wa akili atoa kali ya mwaka hospitalini


Na Mashaka Mhando, Korogwe

MKAZI wa Korogwe, mkoani Tanga ambaye inadaiwa alilazwa katika Hospitali ya Wagonjwa wa Akili Lutindi, wilayani humo,
hivi karibuni alitoa kali ya mwaka baada ya kutoka wodini, kuingia katika gari ambalo dereva wake alikuwa hajalizima na kuondoka nalo akiendesha mwenyewe.


Tukio hilo lilivuta hisia za watu wengi waishio jirani na hospitali hiyo, ambapo dereva wa gari hilo alifahamika kwa jina moja la Bw. Wikama ambaye aliliacha gari hilo likiwa halijazimwa.

Akizungumza na gazeti hili, Diwani wa Viti Maalumu Tarafa ya Bungu, Bi. Elizabeth Singano, alisema mgonjwa huyo wa akili ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja, aliendesha
gari hilo na kushuka nalo katika milima yenye miteremko mikali
yenye kona bila wasiwasi wowote.

“Ilibidi zipigwe simu ili kuomba msaaada wa kulizuia gari ndipo wananchi waliamua kuweka magogo barabarani ili kulizuia,” alisema Bi. Singano anayekaa kitongoji cha Bethelehemu
kilichopo jirani na hospitali hiyo.

Aliongeza kuwa, Bw. Wikama alifika katika kituo hicho baada ya kupeleka mgonjwa wa akili na alipoteremka kwenye gari hakulizima ndipo mgonjwa huyo aliingia na kulichukua.

“Watu walishtuka walipoona mgonjwa wa akili akiendesha gari, walianza kupiga kelele wakati akiondoka nalo lakini mwenyewe hakuonesha waziwasi wowote,” alisema.

Majira lilipomtafuta Bw. Wikama ambaye ni mkazi wa Donge, jijini humo kwa njia ya simu ili kuzungumzia mkasa huo, alikiri kutokea tukio hilo na kudai kuwa, asingependa kulizungumzia kwa kina kwani gari hilo ni mali ya ofisi si la kwake.

“Ni kweli bwana mgonjwa wa akili aliendesha gari nililokwenda nalo hospitali ila nisingependa kulizungumzia sana tukio hilo, wapo watakaolipokea tofautina,” alisema Bw. Wikama ambaye alipotakiwa kutaja namba za gari na aina yake alikata simu
na alipopigiwa tena hakupokea.

Hata hivyo, Ofisa Utawala wa hospitali hiyo aliyefahamika kwa jina moja na Bw. Lauth, alipoulizwa kuhusu tukio hilo alikiri kutokea kwa tukio hilo na kudai mgonjwa huyo wamemrudisha Dar es Salaam.

Alisema tukio hilo halikuwa la kawaida lakini limetokea kwa sababu aliyefika na gari hospitalini hapo hakulizima kama ilivyo kawaida ya madereva wanaopeleka wagonjwa ili kuepuka matukio ya aina hiyo.


44 comments:

  1. HIKI NI KITUKO CHA KUANDIKWA KILICHOTOKEA DUNIANI KWANI ANAYEJUA LUTINDI KULIVYO HATA DAREVA KAMILI LAZIMA AWE MWANGALIFU SIO SUALA LA KUZUNGUMZA KIUDAKU AU UMBEA KAMA GARI LINGEACHA NJIA UKO UWEZEKANO HATA NYAMA ZA DEREVA ZISIONEKANE

    ReplyDelete
    Replies
    1. Open Letter From Valerian Family!
      Dear all in the name of Jesus our Lord and savior.

      I have been keeping quiet for some times, but Jesus calls us all to use our intuitions and speak out the truth and only the Jesus kind of truth that he died on the cross for. I'm Valerian Family member and I had the greatest opportunity to talk to him every other Sunday, and I saw him in his last days fading away. It was the hardest thing to see a fellow human being going through. Only Lord God Jehovah can understand the pain and anguish of his passing, yet the kind of things this young family is going through, sadly from the very people who are suppose to guide and protect this young family.

      The history is as bad to the point that Some Balthazar Family members got so hateful and jealous to ask publicly "Why there is no death in the Valerian's Family? OR "why none of the Valerian's children are dying like ours?". This is kind of things that growing to this level can lead such hatred to deceive people and take matters on their hands to cause death, as they wish it so bad. But what they dont understand, there is God and that the widow, Mama Pendo, was a nurse first before she became a teacher, who could health identify problems of her kids at very early stage and seek medical treatments. While some family members, possibly, were going for traditional medicine and possibly let sickness grow on to their children beyond repair. But when faith is involved you cannot just fade it away as simple as i explained above, or just wipe out the decades of hatred. We need help and that help is from the institution like yours. More payers and God given guidelines. We need it desperately.

      We have a problem. It is problem rooted in the Chagga People Tradition of invading widows' home and oust them and their children to fend for themselves after the father, head of the family as God divinely granted them, passes away. This is done without remorse and no one, even the most educated and or exposed to the Western Civilization Culture life style are doing it and or witnessing it in their own families and don't say or do a thing about it, in spite of their knowledge that is not the right thing to do. It is bothering because I know my mother in-law and I know Auntie Florentina Masawe and Bernadin Marselian Masaawe and I have see and studied their moves. There is an issue of Uru People against Women from Marangu and married in Uru. It is hateful and dangerous and need your and our attention all
      This instrument of spreading the word of God can be used wisely and justly to become an agent of change and change that is needed now. Unfortunately, the laws are so vague and have so much gray area that the devil is using them to advance the oppression against widows and the vulnerable.

      You see, God gave us everything to better our relationship with him, but the devil as master minder, manipulator in chief, lair, master musician, master negotiator and destroyer, uses the same world we were given by God through the free-will, including laws and traditions, to destroy us. That is the truth and that is the Jesus Kind Of Truth that Jesus was Crucified for on the Cross and ultimately die for, so we can be salivated. Understanding the truth and the world that we are living is the key path to God in Heaven.

      Please, visit this Link here and evaluate all the facts by yourself and see how God sent you to help in this. We need prayers because this is the spiritual warfare that need prayers than just laws, rules and regulations. The devil is riding up in here hard and we need all the prayers we can get. http://florentinamasaweinvadesvalerianhome.blogspot.com/

      God is great and keep on the good job of God. A we say Amen!!!!!!!!!!!!!


      Hope, on Behalf of Valerian Family.

      Delete
  2. So Amizin,mgojwa wa akili anawezaje kujua hadi kuingiza na kutoa gia? mi naona kama alikuwa mwezi mchanga ssa yuko poa.

    ReplyDelete
  3. du huyo mgonjwa kiboko,yaani akili zake ziko imara kwenye kuendesha magari, lakini kwenye vitu vingine haiko imara

    ReplyDelete
  4. HUYO SIO MGONJWA ANA PEPO TUU MLETENI TUMCHAPE NA DAMU YA YESU

    ReplyDelete
  5. Hiyo ni Bab kubwa inabidi mgonjwa huyo aingizwe kwenye rekodi ya Dunia ya kuwa mgonjwa wa akili mwenye kipaji maalumu.

    ReplyDelete
  6. Nyie madereva fuateni sheria na kanuni za udereva bora bila ya uzembe ulioufanya hayo yasingekutokea, pole sana kaka.

    ReplyDelete
  7. dah kweli hiyo ni kali ya mwaka, washukuru tu Mungu hakuna kibaya kilichotokea hlf labda kabla hazimruka jamaa alikuwa ni dereva ndio maana haikuwa yy kubadilisha gia.

    ReplyDelete
  8. Inabidi madereva wawe care maana huyo mgonjwa angeleta disaster kubwa

    ReplyDelete
  9. huyo dereva anyang'anywe hiyo gari apewe huyo chizi.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mkuu naona na wewe si bure...kweli mtu timamu apokonywe gari then apewe pungwani? tuwe tunatoa comments za kujenga sio ilimradi umetoa

      Delete
    2. Huyo dereva ni mzembe sana apewe karipio kali vinginevyo ipo siku makubwa zaidi yatamkuta.

      Delete
  10. hii inatoa picha kamili ya madereva tulionao hapa nchini.nb, minaona jamaa kama alikuwa anataka kujipima kama akili iko sawasawa au la!josefatd@yahoo.com

    ReplyDelete
  11. Kwa tukio hili inathibitisha kwamba hata mgonjwa wa akili huwa timamu kwa baadhi ya matendo ndiyo maana hata mahakamani mwendawazimu anawezatoa ushahidi na ukapokelewa ilimradi tu mahakama ijiridhishe kuwa japo ni mwendawazimu lakini anautambuzi wa kujua anachokishuhudia ni cha kweli,na hujaribiwa kwa kuhojiwa maswali kadhaa kuona kama anautambuzi.
    Na mwisho nichangie kwa kusema tusifanye vitu kwa mazoea bali tufuate taratibu.maelekezo nk katika kutenda kazi zetu mbalimbali

    ReplyDelete
  12. Huyo yawezekana ni dreva aliyekosa ajira ikabidi ajifanye mgonjwa lakn uzalendo ukamshinda akaonesha ujuzi wake.achunguzwe.(kibongo, aundiwe kamati ya uchunguzi na wenye nchi)

    ReplyDelete
  13. alikuwa ana jitest kama dawa alizopewa zinafanya kazi

    ReplyDelete
  14. Nadhani huyo dereva alikuwa kichaa zaidi kuliko aliyeondoka na gari. Huyo dereva tahira alikuwa na maana gani kuacha gari halijazimwa kwenye eneo kama hilo? Serves him right!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wewe ndo umesema. Dereva ndiye alikuwa na makosa kuliko kichaa mwenyewe. Madereva kuweni waangalifa wakati wote, on stopping the car always turn off the engine and remove the ignition key, sawa bwana?

      Delete
    2. wanaoendesha magari wapo wengi lakini MADEREVA ni wachache sana. kaka nenda haraka NIT ili nawe uwe DEREVA.

      Delete
  15. Huyo atakuwa ni MOGONJWA WA AKILI TIMAMU, yaani mental fresh.

    ReplyDelete
  16. ya jamaa yaani akaamua kuwaletea zilezile za uzembe wa wafanyakazi wa serikali na akaamua kujifanya chizi! nae ukute ni mfanyakazi serikalini!

    ReplyDelete
  17. Nyie waandishi fanye hima huyo dereva ajulikane na mwajiri wake kwani bwege kweli anaweza leta madhara zaidi. Si mnakumbuka ile ishu mtu na mke wake walipo patanishwa baada ya muda jamaa akauwa?

    ReplyDelete
    Replies
    1. huyo mgonjwa wamuajiri mana yuko fit

      Delete
  18. DU!HUYO DREVA NI WA UKWELI YAWEZEKANA ALIKUA NA CLASS C HUYO AWE ANAENDESHA GARI LA MACHIZI WENZAKE AAJILIWE PALEPALE HOSPITALI KUFATA MACHIZI WENGINE

    ReplyDelete
  19. mmh huyo kichaa noma, na kwa nini dereva aliacha gri bila kuzima?alikuwa anakusudia nini?afungwe

    ReplyDelete
  20. Anatisha huyo chizi!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  21. Huyo dereva anastahili adhabu huo ni uzembe ,nakumbuka pale Mwembe Yanga Dsalaam iliwahi kumtokea dereva mmoja aliacha gari ikiwa kwenye moto akaenda kununua chips mara akaja mwizi akaondoka nalo jasho lilimtoka bahati yake tu alipata msaada wa watu wa bodaboda

    ReplyDelete
  22. Tunajifunza tumwombee apone yule mgonjwa ili siku moja aendelee na kazi zake za kila siku. Dereva pole sana mengi yamesemwa lakini inatokea. mimi nakusihi uwe makini kwani hakuna aliyekamilika.. wote walioandika kuna wakati wamewahi kufanya makosa kwa njia moja au nyingine..Bwana Yesu aliyemkamilifu asifiwe! Amen!.

    ReplyDelete
  23. Na wewe nae, umeanza vizuri,hata walo toa comments huenda wamekwisha fanya au watafanya makubwa kuliko hilo, ni MUNGU PEKEE NDIYE MKAMILIFU. rekebisha.

    ReplyDelete
  24. Jamani msione kuwa hao viraza hawajasoma,wamesoma from the TITLE up to the INDEX,ila walichizika coz wamekosa job!ninachomshauri huyo suka asiwe na wasiwasi kwani huyo ni suka mwenzake la zaidi tumuombee asafifiri salama na arudi salama usikute kawafuata machizi wengine ili wampe company usijali atarudisha gari lako

    ReplyDelete
  25. Umewahi kuona familia kama hii?mtu ni mweusi hadi akiangalia kioo kinaandika PLEASE WAIT.....,dada zake ni wabaya hadi wameweka bango getini kwao kuwa ukioa mmoja unapata wawili bure,kwao ni wengi hadi mtoto wa mwisho anaitwa etc,damu zao ni tamu hadi mbu wabeba vitafunwa kama vitumbua,kwao ni wengi mpaka baba yao akiingia anasema hamjambo wananchi,kwao ni kuchafu mpaka kunguni na mende wanavaa gumbut,yaani hata me nmeshindwa kushangaa jamani!!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  26. HAHAHAHAHAHAAAAAAAA HUYO CHIZI NI NOUMAAAA KWAKWELI MADEREVA YAWAPASA KUWA MAKINI JEE HILO GARI LINGEIBIWA INGEKUWAJEEEE SO MADEREVA 2WE MAKINI....rkaswiza@yahoo.com

    ReplyDelete
    Replies
    1. DEREVA apelekwe CHUO CHA USAFIRISHAJI akafundishwe MAADILI ya UDEREVA ili siku nyingine asikubali kuendesha GARI la KUSITUA najua wengi watamlaumu DEREVA lakini SEREKALINI hawatengenezi MAGARI. akijua wajibu wake vizuri kupitia NIT hatokubali tena kuendesha GARI BOVU.

      Delete
  27. Punguani ni yule mwenye gari.aliyeendesha ni mzima kabisa

    ReplyDelete
  28. madereva tuwe care hasa ktk sehemu km hizo majanga yakitokea yatatuathiri, bt tushukuru tu mungu kutuepusha na balaa lolote

    ReplyDelete
  29. Mgojwa wa akili ametumia akili zake kwa akili na mwenye akili hakutumia akili zake kwa akili!!!

    ReplyDelete
  30. Huyu Mwandishi Mhando alichokieleza hapa na uhalisia wa tukio lenyewe ni tofauti. Mimi Nashukuru nilikuwapo. Huyu Mhando alikuja wiki 3 baadae, akifuatana na huyu diwani ambaye ndiye anamjua huyo dereva na wala huyu diwanihakuwapo siku hiyo.

    Kifupi ni Kuwa gari zilikuwa mbili. Moja toka Dara ndio ilikuwa na mgonjwa iliongozwa na ya huyu Wikama. Kufika hapa Lutindi hii gari ya dar ilipasuka cooling system ikawa kama imeshika moto (moshi mwingi sana kutoka kwenye boneti), kumbuka gari zote zilikuwa kwenye "silence" baada ya kumaliza mlima mkali na ziliegesha NJE ya ENEO la hospitali.

    Wikama alichupa kumwokoa dereva mwenzie na tatizo ka gari yake. Hapo hapo ndipo huyo kijana wa KISOMALI alirukia gari na kuondoka nayo.

    Walimfuata na gari hii ya pili na kumdhibiti na dereva Wikama tena ndiye aliokoa maisha ya Msomali huyu asiuwawe na watu wenye hasira

    Mwandishi Mhando kasahau kuiuliza hospitali ni vipi "mgonjwa" wao hakuwa ndani ya hospitali. Huu ni ubabaishaji.

    Gari husika ni mali ya huyo Wikama na ni gari binafsi, na sote tulishuhudia. Sasa huyu bwana Mhando hizi hadithi anajua kazitoa wapi. HAKUWAPO.

    ReplyDelete
  31. Ndugu yangu ahsante sana kutuelimisha upande wapili wa mkasa huu. Nikiipitia hii makala ya Mhando kwa kweli hata mimi naona mashimo. Kaanza kwa kusema "mkazi wa korogwe" wakati hospitali imesema ilimrudisha "dar-es-salaam" Sasa mkazi wa korogwe anarudishwa vipi Dar?

    Pili huyu Mhando yaelekea ni kweli alifika hospitali na kuongea na huyo afisa lakini kwa dereva mhusika anaelekea kuridhika kupiga simu tu na inaelekea hawakujibizana vizuri. Kama Mashaka anakaa Tanga na huyu dereva anakaa tanga mjini tatizo la kumtafuta kuonananaye ana kwa ana lilikuwa wapi?

    Nakubali kuwa dereva anatokewa na hali ya dereva mwenzake kuwa katika hali hatarishi lazima atahaha kuokoa maisha ya dereva mwenzake. Ni ajabu Mhando hajaandika kiungo hiki katika hadithi yake kwa vile hajui na pia HAKUWAPO.

    Lakini ni kwanini hospitali haikuulizwa ni vipi mgonjwa wao ashambulie gari hii nje ya uzio wa hospitali? wao walikuwa wapi?

    Nashukuru kujua alikuwa ni kijana wa kisomali na alishamaliza tiba akisubiri kurudi kwao. Hii ndio maana aliweza kuendesha gari bila madhara.

    ReplyDelete
  32. Ahsante sana mtowaji maoni wa pili toka mwisho. Amelaumiwa dereva kwa kejeli kibao bila kufahamu ukweli wa tukio. Hii imetokana na muandishi m'babaishaji, na ndio maana wakati mwingine wanafungiwa au kusitishwa wasiandike kwa sababu za kubuni buni habari na hali uwezekeno wa kumfikia mhusika upo isipokuwa uvivu au uzembe. Driver kawa mzembe kwa ajili ya makala mbovu, lakini ninachotaka kusema ni kwamba mgonjwa awe muandishi sio msomali, maana kukurupuka ukaandika habari zisizo na ukweli ni kosa la jinai unaupotosha UMMA. Waandishi heshimni kazi yenu maana nyie ndio wapaliliaji njia na wasomaji hufuata nyuma yenu. Poleni wooote mlie potoshwa na mwanahabari wetu. Ahsanteni mbarikiwe AAAAAMEN

    ReplyDelete
  33. I visited several web pages however the audio quality
    for audio songs existing at this website is truly fabulous.

    ReplyDelete