15 March 2013

Papa Mpya: Nimeanza kazi rasmi



ROAMA, Italia

PAPA mpya wa Kanisa Katoliki duniani, Francis I, ambaye ni wa kwanza kuchaguliwa kutoka Amerika ya Kusini, ameanza kazi
rasmi akitangaza kulileta kanisa hilo pamoja.


Baada ya uchaguzi huo, jana Papa Francis I, alitembelea Kanisa la Santa Maria, mjini Roma na kufanya misa maalumu ya maombi.

Papa Francis I, alitumia ibada hiyo kumuombea mtangulizi wake Papa Benedict XIV na kutoa wito wa kuimarisha udugu miongoni mwa waumini wa kanisa hilo.

Kwa mujibu wa Kituo cha Televisheni cha Aljazeera, kimesema kiongozi huyo ambaye jina lake kamili ni  Jorge Mario Bergoglio (76), kutoka nchini Argentina, atakuwa Papa wa 266 katika kanisa hilo duniani.

Awali alikuwa Askofu Mkuu wa zamani wa Jimbo la Buenos Aires nchini humo ambapo baada ya misa ya jana, alisema tayari ameanza kazi kama Mkuu wa Kanisa hilo lenye waumini bilioni 1.2 duniani kote.

Wakati huo huo, salamu za pongezi zinaendelea kutumwa kutoka mataifa mbalimbali ulimwenguni juu ya uteuzi wake ambapo Waziri Mkuu wa Australia, Julia Gillard, alisema kuchaguliwa kwa kiongozi huyo ni tukio la kihistoria duniani.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. Ban Ki Moon, naye ametuma pongezi zake kwa Papa huyo na kumtakia mafanikio mema. Viongozi wengine waliotuma salamu za pongezi ni Rais wa Argentina Cristina Kirchner na Rais wa Marekani, Bw. Barack Obama aliyedai Bergoglio ni mtetezi wa masikini na wanyonge.

Siku yake ya kwanza ofisini kama Papa Mtakatifu, anatarajiwa kuwateua wafanyakazi wakuu ambao waatamuhudumia chini
ya uongozi wake na kufanya misa nyingine katika Kanisa
la Sistine, mjini Roma.

Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), lilidai uteuzi ambao atufanya kiongozi huyo utakuwa ishara ya mageuzi katika uongozi uliozongwa na kashfa nyingi na kuonesha mwelekeo mpya.

Pia kiongozi huyo anatarajiwa kukutana na vyombo vya habari
katika mkutano maalumu ili kuelezea mikakati yake kwa kanisa
ambapo Machi 17 mwaka huu, ataongoza misa ya kwanza.

No comments:

Post a Comment