18 March 2013

TAKUKURU kushirikiana na asasi za dini

Na Rehema Maigala

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)wameungana na asasi za dini katika kuzuia na kupambana na rushwa Tanzania.

Akiweka jiwe la msingi jana katika Baraza la Misikiti Tanzania (BAMITA)  Mkurugenzi mkuu wa TAKUKURU Edward Hosea alisema,kila asasi zote za dini zinatakiwa tuungane kwa pamoja ili kulipiga vita suala la rushwa.

"Sisi kama TAKUKURU tunampango wa kuhusisha taasisi zote za dini na vijana ili kupambana na rushwa kwani ni adui wa haki"alisema Hosea

Aliongeza kuwa rushwa ndio chanzo kikubwa cha kuleta umasikini katika Taifa letu hivyo ni vizuri pia na asasi za dini ziunge mkono suala hili.

Vilevile alisema hivi sasa wameamua kupitia katika asasi za dini baada ya kuona viongozi wa dini wanakutana na watu kila siku kwa ajili ya kuwafundisha maadili mema hivyo ni vizuri waunganishe na wakemee suala la rushwa.

"Kuubiri kwa viongozi wa dini nadhani ujumbe utafika haraka kwa kuwambia waumini wao kuwa rushwa ni dhambi na atakayetoa au kupokea rushwa hatofika mbinguni kamwe"alisema Hosea  

No comments:

Post a Comment